MCF Redio; Redio Mashuhuri ya Kiinjilisti Nyakati Zote

Katika mitandao ya intaneti, kuna namna ambavyo mahariri ya kivideo ama ya sauti yanavyopeperushwa moja kwa moja hadi kwenye tarakilishi ama kifaa chochote kinacho uwezo wa kusoma tovuti. Mjini Kampala, Uganda; kuna mwamko mpya sasa katika mlengo wa redio ya injilisti inayofanya matangazo mtandaoni. MCF Redio ni mojawapo wa stesheni za kutangulia kwa kupeperusha matangazo ya injili ikitumia mtandao kwa hisani ya Mutundwe Christian Fellowship.

Idhaa hii inarusha mahubiri ya Mchungaji Tom Balaba Mugerwa ambaye ndiye kiongozi mashuhuri wa kanisa la Mutundwe Christian Fellowship lililoko Kaabawa huko Mutundwe jijini Kampala, nchini Uganda. Isitoshe, MCF Redio wamejenga tovuti zinazofanya katika simu za mkononi halimashauri ‘Android’ na ‘iOS’ ili kurahisisha au kunyoosha matangazo ya injili moja kwa moja mtandaoni. Idhaa hii ilipoanza miaka sasa imepita nne, mtindo huu ulikuwa mbichi kwani si stesheni nyingi zilizoweka mapeperusho mtandaoni, mbali hata zile za injili zilikuwa tu hewani kama kawaida.

Kanisa hili la Mutundwe Christian Fellowship linalotoa huduma ya MCF Redio; lilipoanza mnamo mwaka 1992, washirika walikuwa wakifanya ibada ya kanisani pale nyumbani kwa Mhubiri Tom Mugerwa. Mungu alipomuita katika huduma ya injili, Mchungaji alikuwa akiishi na kufanya kazi jijini London, Uingereza. Alipopata ishara ya Mola ya kumshauri arudi nyumbani Uganda ile amjengee kanisa; aling’ang’ana na jambo hili na kulikataa kwa mda, ijapo hakupata amani na hadi akapata maradhi na kulazwa hospitalini. Hadi alipokubali na kuitii amri yake Mungu, ndipo Mhubiri Tom akafunga virago vyote na kurudi Afrika ya Mashariki.

Alipowasili nchini Uganda, Mhubiri Tom Mugerwa aliuongoza mkutano ule wa nyumbani palipo pia bibi yake Mhubiri Justine Mugerwa hadi idadi ikawa imeongezeka mno. Mikutano iliyokuwa ni ya Ijumaa pekee hapo awali ikazidi hadi Jumatano tena hata usiku kucha; kesha ikaanza kutendeka pale nyumbani na ikawa kuta zake haziwezi kustahimili tena ule umati. Hapo ndipo walijenga kijumba cha kwanza kilichokuwa kimeezekwa na aina ya mafunjo pale nje ya nyumba ya Mhubiri. Miaka kadhaa baadaye ikawa hata kile kijumba cha mafunjo nacho hakitoshi tena, na mwelekeo sasa ukawa ni kanisa rasmi lijengwe wakitumia mbao.

Mnamo mwaka wa 2002, kanisa lile la mbao likawa pia halitoshi kwani waumini waliongezeka maradufu. Kanisa liko sasa katika ploti nambari 33 barabara ya Kiyimba pale Mutundwe, Kampala; ndilo lenyewe walilojenga Mutundwe Christian Fellowship mwaka ule. Mhubiri akiwa na waanzilishi wenzake watano walifanya juhudi kulingana na vile Mola alivyowawezesha kutekeleza majukumu ya injili ingawa panapo shida nyingi ambazo ziliwakumba. Waliendelea hadi kanisa la Mutundwe likawa na stesheni yake binafsi kuliwezesha kufikia umati zaidi katika jiji la kampala na mitaa inayolizunguka; nayo ni MCF Redio.

Katika mtandao wa intaneti, programu za kuvuta sauti na video kwa mbio za hadi 512Mbps zimepata maarufu hivi majuzi. Katika programu hizi halimashauri ‘applications’, zinayotumia teknolojia ya ‘webcasting’; huduma na ujumbe wa vifaa kama MCF Redio zinapatikana panapo mtandao wa intaneti. Redio nyingi mtandaoni zinalitolewa na stesheni zilizopo tayari zikipeperusha matangazo hewani, ilhali wanatumia kipande kimoja cha idhaa kufanya matangazo mtandaoni. Mifano kadhaa ya zile huduma za kuvuta mtandaoni ni kama; YouTube, Facebook Live na zinginezo ikiwemo programu ya Redio Injilisti MCF.

Umaradufu wa teknolojia hii umeimarishwa na tabia za wasafiri katika nchi za mbali wakihitaji kupata stesheni za redio kutoka nchi zao za nyumbani. Hawa wasafiri, ama mtu yeyote akiwa mahali popote; anaweza kuingia mtandaoni na kuiskiza idhaa anayeipendelea akitumia tovuti, halimashauri ‘browser’ ama programu spesheli inayobeba matangazo ya ile stesheni. Wasikilizaji pia wanaohitaji huduma zisizo za kawaida ama nje ya zile ninazopatikana hewani, wako na nafasi ya kuzipata wakitumia vifaa mtandaoni ambavyo vinavyokaribia kufanana na redio ya kawaida. Matangazo mengi ya redio za mtandaoni huwa yakifanyika moja kwa moja ama kurekodiwa; na haziwezi kusimamishwa ama kurudishwa nyuma wakati zikiendelea kurushwa.

Huduma katika ibada za Mutundwe Christian Fellowship zinajihusisha sana kwa mikutano ya waumini katika jukwa zozote zile ili kupasha injili ya yesu kristo. Ukombozi kutoka kwa minyororo haswa ndilo jambo ambalo kanisa hili linabobea kwani mhubiri Tom anacho kipawa cha kuyatorosha mapepo machafu yanayohangaisha wanadamu. wajane pia wanayo huduma inayojali maslahi yao katika kanisa hili, wengi wa washirika wakiwa wahudhuria mikutano midogo ya nyumba kwa nyumba halimashauri ‘home cells’. Zaidi wahudumu wa Mutundwe Christian fellowship wanawajali walioko hospitalini na magerezani ili kuwapa motisha na moyo ulio na matarajio ya maisha mema; ilhali wakimfahamu Yesu Kristo.

Jinsi mapeperusho ya injili hii inapotekelezwa katika MCF Redio mtandaoni kwa tovuti la kanisa la Mutundwe pamoja na lile. Katika tovuti hili kuna ‘MCF Radio’ itakayoleta mahubiri, matangazo na hata nyimbo za injili. Huduma itaanza kukujia ikipitia kifaa ambacho unatumia iwe ni kompyuta ama simu ya rununu.  Pale pia kuna namna ya kuwasiliana katika gumzo la moja halimashauri ‘live chat’ ambapo msikilizaji anaweza uliza swali, peana himizo au achangie katika soga la majadiliano yanayoendelea.

Kipindi hiki ni cha mwisho hapa duniani, na mambo mengi yamekuwa magumu zaidi kwake binadamu; na halisi kwa mkristo. Majanga ya njaa na vita vikali yanaoangamiza wengi, wakristo kuteswa na uchawi kuongezeka ni ishara ya kwamba shetani ameimarisha jitihada za mapambano na maangamizo akitaka nyoyo za binadamu. Nafsi ya Mhubiri Tom Mugerwa itafurahia wakati mwanadamu ataweza kupaa mahali pake halisi katika jeshi lake Mwenyezi Mungu ili kuiendesha vita dhidhi ya mwovu shetani na jopo lake.

Mhubiri Tom katika ibaada za MCF Redio ameweza kuwavutia wengi watoto kwa vijana na hata watu katika ndoa. Wanasiasa pia, wafanyi kazi katika huduma ya Bwana; na hata wale walio katika sekta za serikali au kibinafsi wameweza kupata injili ya neno la Yesu Kristo kupitia MCF Redio mtandaoni. Wengi ni wale Wakristo ambao wametoa ushuhuda wa kutosha kulingana na vile ambavyo mwelekeo wa maisha yao umebadilika hadi waliskie neno la injili kupitia Mhubiri Tom akipitia katika idhaa za MCF Redio.

Mhubiri pia ameandika vitabu kadhaa na kurekodi mafunzo yake kwa kanda za ‘video’ au sauti pekee. vitabu hivi ni baadhi yake ni ‘Agano la Mungu’, ‘Kumplekea Shetani Vita Kwake’, na ‘Kuwa Mwema katika Yesu’. kitabu cha ‘Shughuli za Roho Mtakatifu’ kiko pamoja na CD ya kumbukumbu ya sauti iliyonakiriwa kwa lugha ya Luganda halimashauri; ‘Ekitibwa kya Mukama’.

Akihariri kuwa Roho Mtakatifu ndiye aliyewezesha kanisa la Mutundwe Christian Fellowship kuongezeka kwa ukubwa na haraka; Mchungaji anasema kwamba imani katika Yesu Kristo imewapa watu wengi matarajio mema, uponyaji na amani iliyo na raha kubwa. Akihubiri kutoka kitabu cha Wakolosai 1:18, Mhubiri Tom Mugerwa anahariri kwamba kanisa ni lake Yesu Kristo kama urithi; na analijali mno na kulitetea katika vita vyote vya kiroho. Haya ni mambo ambaye Mchungaji ameshuhudia maishani mwake humu akisema wito wake ni neno la bwana liangaze kote duniani, na hisani hii inamsukuma sana kuiimarisha injili kuwezesha Mungu kuliongoza Kanisa Lake.

Biblia takatifu inasema kuwa “Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka; Yohanna 4:23. Huduma za MCF Redio zinaimarisha uabudu huu kwa nia na njia kwani inafikisha injili kwa wale wanaoihitaji na ikitumia njia ambaye ni rahisi pia tofauti sana sana ili ifikie vijana barubaru ambao hawasikilizi redio ya kawaida. Bila shaka, njia hii imeipa Mutundwe Christian Fellowship umashauri katikati mwa redio zingine za injili mjini Kampala, Uganda; Afrika nzima na hata ulimwenguni kote. Wengi wanafurahia sana jinsi ukiwa hata na simu ya rununu iliyo bei rahisi utaweza kupata mapeperusho ya MCF Redio.

Vipindi vya Kiinjilisti katika MCF Redio vinatayarishiwa pale Mutundwe Christian fellowship na zinalingana na vile ambapo kanisa linaendeleza huduma. Kanisa lenyewe liko wazi kwa yeyote yule atakayehudhuria kutoka asubuhi hadi usiku. Ibada inaendelea kanisani kutoka Jumatatu asubuhi saa mbili unusu hadi saa kumi unusu ya jioni, kisha kutoka saa mbili hadi saa kumi. Masaa ya usiku kunayo ibada ya kuwaombea wachungaji na wahudumu. Jumanne na Alhamisi asubuhi ibada inaanza saa tano unusu hadi saa kumi unusu na ndipo usiku maombi ya ukombozi yanafanyika kutoka saa mbili hadi saa nane na nusu ya usiku.

Jumatano nayo mchana ina masaa ya ibada kama ya jumatatu na yale ya usiku ni kama Jumanne na Alhamisi. Ijumaa ibada ni za kutoka saa mbili unusu hadi saa kumi na nusu mchana, hali usiku ni kesha rasmi inayoanza saa mbili za usiku hadi kesho yake asubuhi. Jumamosi washirika Katika Mutundwe Christian Fellowship wanakutana kwanzia saa sita adhuhuri hadi saa kumi na moja unusu ya jioni. Jumapili baada ya ibada ya misa, washishirika wanatembea mlango hadi mwingine katika huduma ya nyumba kwa nyumba. Hii mipangilio yote inaidhinishwa katika MCF Redio mtandaoni ili kujulisha washirika na wageni jinsi ya mfuatilio wa ibada, huku wakipata ibaada zinginezo zikiwa pamoja na nyimbo za Kiinjilisti na kumsifu Mungu.

Sikiliza MCF Redio mtandaoni upate injili inayorushwa kidijitali na kwa ubora kama runinga; kwa masaa ishirini na manne kila siku. Tembelea mtandao wa Mutundwe Christian Fellowship ama caster.fm na wakati wowote; ilhali toa programu kwenye ‘Play Store’ au ‘App Store’ upate matangazo, taarifa na arifu zinginezo katika simu ya rununu. Mahariri ya mahubiri yake Mchungaji Tom Mugerwa itakupa moyo na kukuelimisha jinsi ya kupata uzima wa milele kupitia kwake Yesu Kristo; na jinsi ya kuishi maisha yanayompendeza Mungu hapa duniani. Shida zozote za laana, machafuko katika ndoa, uchawi na nguvu za giza katika maisha yako zitashindwa unapohudhuria taarifa za injili katika MCF Redio mtandaoni.

Views: 1

Comment

You need to be a member of The Brooklynne Networks to add comments!

Join The Brooklynne Networks

Brooklynne.net- Financial Services for Businesses and Professionals

© 2019   Created by Brooklynne Networks.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

tag.